Burundi yaionya Rwanda huku mzozo Kongo ukiendelea kutokota
13 Februari 2025Hayo ni kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo pamoja na vya mashirika ya kiutu. Miji iliyotekwa ni Ihusi na Kalehe, iliyoko karibu kiliomita 60 kutoka Bukavu.
Katika taarifa, serikali ya Kinshasa imeitisha mkutano wa dharura wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika - SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki - EAC kutathmini hali hiyo na "kutathmini hali na matokeo ya kitendo hiki kipya cha uchokozi", ikitoa wito wa vikwazo. Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye amesema yeyote atakayeishambulia nchi yake naye atashambuliwa.
Wakati huo huo, viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Kongo na ule wa Kanisa la Kristo la Kongo umekutana na waasi wa M23 mjini Goma katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kusaka amani na mazungumzo. Walikutana na kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23 Corneille Nangaa.