BurkinaFaso na Mali zasusia mkutano kuhusu ulinzi
26 Agosti 2025Burkina Faso na Mali zimejizuia kutuma wawakilishi wake katika mkutano kuhusu masuala ya kijeshi barani Afrika unaoendelea nchini Nigeria.
Mali na Burkinafaso zinazoongozwa na tawala za kijeshi bado hazina mahusiano mazuri na majirani zake katika kanda hiyo ya Afrika Magharibi.
Kwenye mkutano huo wa wakuu wa majeshi barani Afrika ulioanza jana Jumatatu mjini Abuja, Niger, ambayo pia inatawaliwa na jeshi, iliwakilishwa na balozi wake, Kanali Meja Soumana Kalkoye.
Mkutano huo utakaomalizika Jumatano umetajwa na serikali ya Nigeria kuwa wa kwanza mkubwa kuwahi kufanyika barani Afrika, unaowaleta pamoja maafisa wa ngazi za juu jeshini kutoka mataifa mbali mbali ya bara hilo kujadili juu ya mikakati ya pamoja na kutafuta suluhisho kuhusu mahitaji ya kiulinzi ya bara la Afrika.