BUNGE LA UJERUMANI
11 Machi 2005BERLIN:
Bunge la Ujerumani-Bundestag,lilijadiliana jana njia za kupambana na ukosefu mkubwa wa kazi nchini Ujerumani.Tarakimu za hivi punde juu ya idadi ya wasio na kazi humu nchini imefikia watu milioni 5.2 na hii ni rekodi tangu kumalizika vita vya pili vya dunia.
Kiongozi wa upinzani wa chama cha CDU Bibi Angela Merkel, aliitumia hotuba yake Bungeni kuitisha kufanyike mageuzi makubwa juu ya soko la nafasi za kazi nchini Ujerumani.
Mwernyekiti wa chama-tawala cha SPD Bw.Franz Münterfering,alimzima kwa kusema hotuba ya Bibi Merkel ilituwama zaidi juu ya mabishano ya kisiasa na kasoro katika kutoa mashauri madhubuti kupiga vita ukosefu wa kazi.
Kanzela Gerhard Schröder atakutana na viongozi wa upinzani wiki ijayo kujadiliana nao jinsi ya kumaliza tatizo hili la ukosefu wa kazi.