Bunge la Ujerumani kupitisha kuzuia kikomo cha ukopaji
18 Machi 2025Friedrich Merz anayetazamiwa kuwa Kansela ajaye wa Ujerumani anaupigia upatu mpango huo akitaka upitishwe na bunge la sasa, akihofia kwamba huenda ukapingwa na bunge lijalo litakaloanza vikao vyake mnamo Machi 25.
Soma pia: CDU/CSU yashinda uchaguzi wa bunge Ujerumani
Mapema leo, Merz alisema kuwa sasa inabidi wajenge upya uwezo wao wa ulinzi kuanzia mwanzo.
''Kwa mkakati wa ulinzi na ununuzi unaoendeshwa na teknolojia, ufuatiliaji huru wa satelaiti wa Ulaya, droni na silaha na mifumo mingi ya kisasa ya ulinzi, na zaidi ya yote, kuwepo kwa maagizo ya kuaminika na yanayotabirika ambayo yanapaswa kuelekezwa kwa wazalishaji wa Ulaya wakati wowote inapowezekana.''
Mpango huo unaotarajiwa kupitishwa na wabunge unalenga kulegeza sheria za katiba na kuondoa ukomo wa kukopa na hivyo kuufufua uchumi wa Ujerumani ambao ndio mkubwa zaidi barani Ulaya.