Bunge la Uingereza kuamua muswada wa huduma ya kifo
20 Juni 2025Matangazo
Iwapo mchakato huo utaidhinishwa hayo yatakuwa mabadiliko makubwa ya kijamii kwenye taifa hilo la barani Ulaya. Novemba mwaka uliopita wabunge walio wengi waliunga mkono pendekezo la kuandaliwa muswada wa sheria ya kuruhusu huduma ya msaada wa kifo.
Baada ya miezi kadhaa ya majadiliano makali, muswada huo utapaswa kuruka kuhunzi cha kwanza hii leo kabla ya kuidhinishwa rasmi kuwa sheria miezi michache inayokuja.
Uchunguzi wa maoni unaonesha raia wengi wa Uingereza wanaunga mkono huduma ya msaada wa kifo.
Chini ya mapendekezo ya muswada huo, wagonjwa wenye akili timamu lakini walio kwenye hali mahututi na wanaokadiriwa kuwa na muda usiozidi miezi sita ya kuishi wataweza kuomba huduma ya uhai wao kukatishwa.