Bunge la Iraq limetoa muda wa siku tatu kuyafumbua masuala yanayokorofisha katiba
23 Agosti 2005Baghdad:
Mswaada wa katiba umewasilishwa bungeni kama ilivyopangwa jana usiku.Spika wa bunge Hajem Al Hassani amesema wakati wa mkutano na waandishi habari, mswaada huo wa katiba haujakamilika.Mada tatu zinabidi zitatuliwe.Mada hizo ni pamoja na muundo wa shirikisho na majimbo yatakayojiamulia mambo yao wenyewe,hatima ya chama tawala cha zamani- Baath na majukumu ya rais,waziri mkuu na spika wa bunge.Mkutano wa bunge uliolengwa kujadili mswaada wa katiba ulidumu dakika tatu tuu.Spika wa bunge Hajem al Hassan amesema mada hizo zinazozusha mabishano zinabidi zipatiwe ufumbuzi katika kipindi cha siku tatu zijazo.Muda mfupi kabla ya kikao cha bunge kufunguliwa,makamo wa rais Ahmed Chalabi aliahidi kura ya maoni ya katiba itaitishwa kama ilivyopangwa october 15 ijayo. Waarabu wa madhehebu ya sunni hawavutiwi na mswaada huo wa katiba na haijulikani kama wataiunga mkono au la kura ya maoni itakapoitishwa..Rais George W. Bush amesifu maendeleo yaliyopatikana nchini Irak.