Bunge jipya ya Ujerumani kukutana kwa mara ya kwanza
25 Machi 2025Matangazo
Kikao hicho kitafunguliwa na Gregor Gysi, mbunge ambaye amehudumu kwa muda mrefu zaidi na atakayeongoza kikao hicho hadi spika mpya atakapochaguliwa.
Muungano wa kihafidhina wa vyama ndugu vya CDU/CSU wa Friedrich Merz, ambaye ni kansela mtarajiwa wa Ujerumani, ulimteuwa mwanasiasa mwenye uzoefu Julia Klöckner kuwa spika ajaye wa bunge hilo.
Kwa kawaida, chama chenye wingi wa viti bungeni ambao katika bunge hilo jipya ni muungano huo wa kihafidhina ndio unaojaza nafasi hiyo.
Spika wa bunge anashikilia wadhifa wa pili wa juu zaidi serikalini baada ya rais wa shirikisho.