Bundesliga: Hamburg yatoa sare tasa, Cologne yapata ushindi
25 Agosti 2025Matangazo
Klabu hiyo iliyopandishwa daraja msimu huu ilitumia muda mwingi kujilinda zaidi katika mchezo wa jana. Hamburg ilikuwa klabu ya mwisho muasisi wa Bundesliga iliyocheza kila msimu tangu ligi kuu ilipoanzishwa mwaka wa 1963, hadi hatimaye iliposhushwa daraja mwaka wa 2018 baada ya kunusurika chupuchupu mara kadhaa.
Klabu nyingine iliyorejea katika ligi kuu msimu huu kutoka daraja la pili, FC Cologne, ilipata ushindi wa 1 - 0 dhidi ya Mainz. Mainz ilibaki na wachezaji kumi uwanjani katika dakika ya 60 baada ya mchezaji wao Paul Nebel kuonyeshwa kadi nyekundu. Cologne walipata bao dakika ya mwisho ya mchezo kupitia kichwa cha Marius Bülter.