Budapest.Mamia kwa maelfu waendelea na maandamano.
24 Septemba 2006Mamia kwa maelfu ya watu wameshiriki katika maandamano katika eneo la jengo la bunge mjini Budapest dhidi ya waziri mkuu wa Hungary Ferenc Gyurcsany ( Djuksanyi).
Waungaji mkono wa chama kikuu cha upinzani cha Fidesz walikuwa miongoni mwa wale waliojikusanya katika uwanja huo.
Viongozi wa chama wamerudia miito yao ya hapo kabla ya kumtaka Djuksanyi kujiuzulu.
Polisi wamesema kuwa walikuwa wamejiweka tayari, kuzuwia marudio ya ghasia za hapo mapema mwanzoni mwa wiki ambapo watu 150 walijeruhiwa katika mapigano baina ya polisi na waandamanaji.
Waziri mkuu Djuksanyi alinaswa katika ukanda wa kunasia sauti ambao ulitolewa kwa vyombo vya habari vya Hungary akiwaeleza wajumbe wa chama chake kuwa alidanganya juu ya urari wa bajeti ya taifa ili kuweza kushinda uchaguzi mwezi wa Aprili.