BRUSSELS:Umoja wa Ulaya walaani ukatili wa polisi.
8 Machi 2005Matangazo
Umoja wa nchi za Ulaya umelaani matendo ya nguvu yalivyofanywa na polisi wa Uturuki dhidi ya wanawake waliokuwa wanaandamana mjini Istanbul jumapili iliyopita. Akizungumza kwa niaba ya nchi za Umoja wa Ulaya,waziri wa mambo ya nje wa Luxumburg bwana Jean Asselborn aliwaambia waandishi habari mjini Ankara kwamba alishtushwa na picha alizoona katika televisheni zilizoonyesha jinsi polisi walivyokuwa wanawapiga mateke na kuwatimba watu waoliokuwa wanaandamana kwa niaba ya haki za wanawake.Hatahivyo maandamano hayo hayakuwa na kibali cha kufanyika.
Uturuki imeahidi kufanya uchunguzi .