BRUSSELS:Ndege za Afrika zapigwa marufuku kutua Ubelgiji
30 Agosti 2005Matangazo
Serikali ya Ubelgiji imechapisha orodha ya mashirika ya ndege yaliyopigwa marufuku kutua kwenye viwanja vya nchi hiyo kutokana na sababu za kiusalama.Hatua hiyo inafuatia, iliyochukuliwa na Ufaransa baada ya ajali kadhaa za ndege kutokea hivi karibuni.
Ufaransa imeyapiga marufuku mashirika sita ya ndege kutua kwenye viwanja vyake.Mashirika ya ndege za mizigo, yaliyopigwa marufuku kutua nchini Ubelgiji ni pamoja na ya Misri,Congo,Libya,Nigeria Ghana,Rwanda na Afrika ya kati.
.