BRUSSELS:NATO kuwa na dhima Iraq
5 Januari 2004Matangazo
Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO yumkini ukawa na dhima ya kutimiza katika ujenzi mpya wa Iraq kipindi cha usoni lakini kwanza imetakiwa imaarishe shughuli zake nchini Afghanistan.
Hayo yametamkwa na Mkuu Mpya wa NATO waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Uholanzi Jaap de Hoop wakati akiwasili kwenye makao makuu ya NATO nje ya mji wa Brussles kushika wadhifa wake mpya.
Amesema lengo la msingi kwa sasa linapaswa kuwa Afghanistan na kwamba bila ya shaka Iraq pia itakuwa katika agenda wakati fulani lakini kwa sasa ametaka kuchukuliwa kwa hatua moja baada ya nyengine.
Umoja huo wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO mwaka jana ulikamilisha mjadala uliodumu kwa miaka mingi iwapo iendeshe shughuli zake kupindukia Ulaya na Amerika ya Kaskazini kwa kushiriki shughuli za kulinda amani nchini Afghanistan kufuatia mashambulizi yaliongozwa na Marekani yalioupinduwa utawala wa Taliban hapo mwaka 2001.