BRUSSELS:Je mazungumzo juu ya Uturuki yatafanyika?
1 Oktoba 2005Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana amesema ana hakika kwamba makubaliano yatafikiwa juu ya mvutano wa kufanyika mazungumzo ya Uturuki kujiunga na Umoja huo yaliyopangiwa kuanza jumatatu ijayo.
Akizungumza na waandishi wa habari wa gazeti moja la Ujerumani Solana amesema Umoja wa Ulaya imekuwa ikuchukua uamuzi juu ya uturuki wakati wa dakika za mwisho.
Hata hivyo Solana ametilia mkazo kwamba mazungumzo hayo hayawezi kutoa hakikisho kwa juu ya Kujiunga Uturuki kwenye Umoja huo.
Austria upande mwengine inasisitiza kwamba mazungumzo hayo yanafaa kuipa Uturuki nafasi maalum ya ushirikiano badala ya kupewa uanachama kamili kwenye Umoja wa Ulaya.
Lakini Uturuki inasema inachoweza kukikubali ni kuwa mwanachama kamili wa Umoja huo na wala sio kinyume chake.
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 25 wanachama wa Umoja wa Ulaya watakutana kujaribu kuondoa tofauti zilizopo miongoni mwao juu ya Uturuki katika mkutano wa dharura utakaofanyika jumapili huko Luxembourg.