Brussels: Waziri mkuu wa Ubeligiji Guy Verhofstadt ameamuru kutumwa ...
10 Januari 2004Matangazo
wanajeshi hadi 190 wa nchi yake mjini Kisangani-kusaidia kuundwa jeshi jipya la jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo."Si opereshini ya kijeshi,ni mafunzo yanayoweza kuzihusisha nchi nyengine pia za umoja wa Ulaya" amesema hayo kiongozi wa serikali ya Ubeligiji akijibu hoja kama uamuzi huo hawendi kinyume na maagizo ya kamisheni ya baraza la Senet yanayokataza kutumwa wanajeshi katika makoloni au himaya za zamani za Ubeligiji.Kamisheni ya baraza la Senet ilitopa maagizo hayo baada ya kufanya utafiti kuhusu mauwaji ya Rwanda ya mwaka 1994.Kwa mujibu wa waziri wa ulinzi wa Ubeligiji wanajeshi hao watapelekwa Kisangani baada ya kutiwa saini mkataba wa ushirikiano pamoja na Umoja wa mataifa wiki ijayo.Serikali ya mpito ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo imeiomba Ubeligiji iisaidie katika kuunda jeshi jipya la taifa kuambatana na makubaliano ya amani yaliyolengwa kumaliza vita vya wenyewe ,kwa wenyewe nchini humo.