BRUSSELS : Wasi wasi Ulaya juu ya uhaba wa madawa ya homa ya mafua
17 Oktoba 2005Matangazo
Tume ya Umoja wa Ulaya imesisitiza leo hii wito kwa mataifa ya Ulaya kuweka akiba ya madaya ya kupambana na homa ya mafua ili kujiandaa kukabiliana na janga la homa hiyo inayogopewa mno.
Ikitowa maelezo mapya juu ya hali hiyo baada ya kirusi thakili cha homa ya mafua ya ndege kuthibitika kuwepo barani humo hapo Jumamosi pia imesema inaweza kuchukuwa hatua zaidi kuihami Ulaya ikibidi dhidi ya ugonjwa huo.
Philip Tod msemaji wa Kamishna wa Afya wa Umoja wa Ulaya amekaririwa akisema hawataki kuonekana kuwa wanatisha watu bali wanatimiza wajibu wao kuzisaidia nchi wanachama kujiandaa na kuratibu maandalizi yao.