Brussels. Wagoma kuongezewa miaka ya kustaafu na mapema.
29 Oktoba 2005Wafanyakazi nchini Ubelgiji wamefanya mgomo wa nchi nzima wakipinga dhidi ya mipango ya serikali ya kupandisha miaka ya wafanyakazi kustaafu kwa hiari na mapema.
Mamia kwa maelfu ya wafanyakazi kutoka katika vyama vikuu vya wafanyakazi nchini humo waliandamana katika mitaa ya mji mkuu Brussels.
Vyama hivyo vya wafanyakazi vinapinga mageuzi hayo ambayo yataongeza miaka ya kustaafu kwa hiari na mapema kutoka miaka 58 hadi 60.
Wanasema kuwa kuendelea kuwatumia wafanyakazi wazee kunazuwia vijana na wale wasio kuwa na kazi kuweza kupata kazi. Waziri mkuu Guy Verhofstadt ameapa kutosalim amri kwa mbinyo wa vyama hivyo vya wafanyakazi kuweza kuanzisha tena majadiliano kuhusu mageuzi hayo, akisema kuwa mkataba huo utabaki kama ulivyo na kwamba mageuzi hayo ni muhimu kwa ajili ya kuepusha mtafaruku mkubwa wa malipo ya uzeeni katika siku za usoni.