BRUSSELS: Virusi wanaosababisha homa kali wagunduliwa kwenye kuku nchini Uturuki
13 Oktoba 2005Matangazo
Halmashauri ya umoja wa Ulaya imethibitisha kwamba virusi waliogunduliwa kwenye kuku nchini Uturuki, ni aina ya virusi wanaosababisha homa hatari iliyowauwawa watu 60 kusini mashariki mwa Asia.
Kamishna anayesimamia maswala ya afya, Markos Kypriano, amesema kuna uhusiano kati ya virusi hao na wale waliogunduliwa nchini Russia, Mongolia na China. Umoja wa Ulaya umepiga marufuku ununuzi wa ndege na kuku walio hai kutoka nchini Uturuki na Romania. Ujerumani imetangaza sheria kali katika mipaka yake na viwanja vyake vya ndege.