Brussels. Virusi vya homa ya ndege vyaingia katika bara la Ulaya.
14 Oktoba 2005Tume ya umoja wa Ulaya imethibitisha kuwa virusi vya homa ya ndege iliyokutikana kwa kuku na bata kutoka Uturuki ni ile aina ya H5N1 ambayo imeuwa kiasi cha watu 60 katika maeneo kadha ya kusini mashariki ya Asia.
Kamishna wa masuala ya afya wa umoja wa Ulaya markos Kypriano amesema uchunguzi umeonyesha kuwa kulikuwa na uhusiano wa moja kwa moja wa virusi hivyo vilivyogundulika hivi karibuni nchini Russia, Mongolia na China.
Hii inakuja baada ya maafisa wa afya wa Romania kusema kuwa wamegundua virusi kwa bata watatu katika jimbo la bonde la Danube.
Kypriano inayataka mataifa ya umoja wa Ulaya kuhifadhi madawa zaidi ya kupambana na virusi hivyo. Umoja wa Ulaya umepiga marufuku uagizaji wa ndege hai pamoja na nyama za kuku na bata kutoka Romania na Uturuki.
Ujerumani imetoa wito wa kuweka udhibiti wa hali ya juu katika viwanja vya ndege na mipakani.