BRUSSELS: Viongozi wa Ulaya wameshindwa kumtetea Papa
24 Septemba 2006Matangazo
Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya amesema amesikitika kuwa viongozi wa Ulaya walishindwa kumtetea Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 kuhusu hotuba yake juu ya Uislamu.Gazeti la Kijerumani “Welt am Sonntag” hii leo limechapisha matamshi ya Jose Manuel Barroso akisema,Ulaya ikipaswa kutia maanani kitisho cha wakereketwa wa kiislamu,wakati huo huo isibabaishe ustahmilivu na aina fulani ya usahihi wa kisiasa unaoweka mbele maadili ya wengine kuliko yao wenyewe. Barroso amesema,tatizo si matamshi ya Papa,bali hisia za wakereketwa.