BRUSSELS :Umoja wa Ulaya waimarisha hinikizo juu ya Iran.
19 Mei 2005Matangazo
Umoja wa Ulaya umeimarisha hinikizo kuitaka Iran iache mpango wake wa nyuklia la sivyo Umoja huo utapeleka shauri hilo kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Ufaransa na,Uingereza pamoja na mkuu wa sera za nje za Umoja wa Ulaya bwana Solana jumanne wiki ijayo, watakutana na wajumbe wa Iran mjini Brussels ili kuzungumzia mpango wa nykulia wa nchi hiyo, hasa baada ya kusema kwamba inakusudia kuanza tena shughuli muhimu za kinyuklia.
Hatahivyo Iran hadi sasa imekuwa inakanusha madai kwamba ina mipango ya kuunda silaha za nyuklia.
.