BRUSSELS: Ulaya itachangia sehemu kubwa ya vikosi
26 Agosti 2006Matangazo
Idadi kubwa ya wanajeshi watakaoimarisha vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon,itatoka nchi za Ulaya.Kwenye mkutano wa mawaziri wa kigeni wa Umoja wa Ulaya,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan,aliahidiwa kuwa nchi hizo zitatoa mchango wa wanajeshi wasiopungua 6,500 hadi 7,000.Inatazamiwa kuwa hadi wanajeshi 15,000 watapelekwa Lebanon.Ujerumani imejitolea kupeleka vikosi vya wanamaji lakini bado haikuamuliwa hasa ni huduma gani za kijeshi zitatekelezwa.Ufaransa inatazamia kuviongoza vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon hadi Februari mwakani,ambapo Italia itapokea dhamana hiyo.