BRUSSELS: Ujenzi mpya wa maeneo yalioteketezwa na Tsunami uchangámke
25 Juni 2005Matangazo
Kwa mujibu wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa,kazi za ujenzi mpya katika maeneo yaliyoteketezwa na Tsunami,miezi sita iliyopita, kusini mwa Asia,zinapaswa kuharakishwa.Umoja wa Mataifa umeonya kuwa kazi ya kurekebisha hasara iliyosababishwa na mafuriko ya Tsunami huenda ikachukua hadi miaka 10.Kiasi ya nchi 90 mbali mbali zimeahidi kutoa jumla ya Dola bilioni 11 kwa mipango ya misaada na ujenzi.Zaidi ya watu 180,000 walifariki katika mafuriko hayo na wengine kwa maelfu bado wanakosekana.Kwa upande mwingine serikali ya Sri Lanka na waasi wa Tamil Tigers nchini humo,wamekubali kugawana msaada wa Tsunami wa Dola bilioni tatu.