BRUSSELS: Tume ya waangalizi kupelekwa Kongo
21 Julai 2006Matangazo
Bunge la Ulaya litapeleka tume ya waangalizi kwa uchaguzi utakaofanywa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Wiki ijayo,tume hiyo ya waangalizi 12,itafuatiliza matayarisho yanayofanywa kwa chaguzi za rais na bunge.Hapo tarehe 30 Julai,wajumbe hao watatazama vipi uchaguzi unaendelea katika vituo mbali mbali vya kupigia kura.Mbunge wa Kijerumani wa chama cha CDU,Jürgen Schroeder ataiongoza tume hiyo ya waangalizi.