Brussels: Muungano wa Ulaya hauna ushahidi kwamba misaada yake ya...
28 Novemba 2003Matangazo
kifedha inaenda kwa Wapalastina wenye siasa kali. Idara inayochunguza vitendo vya udanganyifu katika jumuiya hiyo huko Brussels imesema hakuna ushahidi kwamba fedha za Muungano wa Ulaya zimekwenda kwa bawa la kijeshi la Chama cha al-Fatah cha Rais Yasser Arafat. Gazeti la Kiengereza, INDEPENDENT, liliripoti kwamba misaada ya fedha kutoka Muungano wa Ulaya , kupitia jumuiya zilioko Ujerumani na Ubelgiji, zimeenda kwa vikosi vya al-Aqsa ambalo ni bawa la kijeshi la Chama cha al-Fatah. Kwa upande mwengine, waziri wa miundo mbinu wa Israel, Joseph Paritsky, ameiomba Ujerumani itoe msaada wa maendeleo kwa Wapalastina. Katika gazeti la FINANCIAL TIMES la Ujerumani, mwanasiasa huyo wa bawa la shoto katika serekali ya Israel alisema sababu ya kufanya hivyo ni maendeleo yanayoonekana katika mwenendo wa amani. Alisema msaada huo utaboresha hali za maisha ya Wapalastina, lakini pia na ya Wa-Israeli.